Header Ads

Header ADS

VIDEO- BEKI APEWA KADI NYEKUNDU BAADA YA KUFUNGA HAT-TRICK SWEDEN

Huko nchini Sweden kunako Ligi Kuu ya nchini humo, beki wa kati wa Norrby IF Medi Dresevic alifunga hat-trick katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Tvaaker na kutolea kwa kadi nyekundu.
Hilo lilikuwa tukio kubwa mno kwa beki huyo, kwani katika maisha yake ya soka rasmi la ushindani amewahi kufunga goli moja tu mwaka 2011 wakati timu yake iliposhinda mabao 3-2 dhidi ya Rosengård.
Medi Dresevic alishangilia goli lake lililokamilisha hat-trick kwa kukimbilia kwenye viti vya mashabiki na kukaa kwa muda huku akijipongeza kwa kujipigia makofi.
Baada ya tukio hilo, kutokana na hapo awali kuwa na kadi ya njano, mwamuzi alimzawadia kadi nyekundu huku wachezaji wenzake pia wakimwakia vibaya kwa kitendo chake kilichopelekea adhabu hiyo.
Adhabu hiyo itapelekea mchezaji huyo kukosa mchezo wao muhimu unaofuata.


No comments

Powered by Blogger.