Barcelona wakamilisha usajili wa Paco Alcacer kutoka Valencia
Klabu ya FC Barcelona ya Hispania imetangaza kukamilisha usajili mshambuliaji wa Valencia Paco Alcacer, FC Barcelona imetangaza kumsajili Paco kwa mkataba wa miaka mitano.
\Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye aliondolewa katika kikosi cha Valencia kilichoshinda bao 1-0 dhidi ya Eibar Jumamosi iliyopita, alifanyiwa vipimo vya afya Barcelona Jana kabla ya kukamilisha uhamisho wake huo uliogharimu euro milioni 30.
Alcacer amefunga mabao 43 katika mechi 124 alizoichezea Valencia huku akiitwa mara 13 kukichezea kikosi chake cha timu ya taifa.
Akihojiwa Alcacer amesema pamoja na kuwa anaondoka Valencia lakini siku zote itakuwa ni klabu ya moyo wake na kuwashukuru mashabiki kwa kipindi chote walichomuunga mkono
No comments