UMEISIKIA HII YA RIO FERDINAND KUWAHI KUOMBA KUSAJILIWA ARSENAL?
Beki kisiki wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand amefichua kwamba kuna wakati alimuomba Arsene Wenger amsajili bure mwaka 2014.
Ferdinand, ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka alijiunga na QPR baada ya mkataba wake na Man United kumalizika kabla ya kustaafu mwishoni mwa msimu wa 2014-15.
Hata hivyo, Ferdinand (37) ameamua kufichua kwamba aliwasiliana na Wenger moja kwa moja, licha kwamba uhamisho huo ungekuwa wa aina yake kutokana na uhasimu uliopo kati ya Arsenal na Man United.
No comments