Header Ads

Header ADS

Zlatan Ibrahimovic ametangaza rasmi kustaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Sweden

Nahodha wa timu ya taifa ya Sweden ambaye aliyekuwa anaichezea klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovic June 21 2016 ametangaza rasmi kustaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Sweden baada ya michuano ya Euro 2016 kumalizika.Screen-Shot-2016-06-21-at-5.19.54-PM
Zlatan ambaye hivi karibuni amejumuishwa katika kikosi ambacho wachezaji wa Sweden watakaoicheza michuano ya Olympic Brazil, ni habari njema kwa Man United ambao wanatajwa kuwa watamsajili baada ya Euro, kwani atakuwa huru na muda mwingi zaidi wa kuitumikia klabu yao.
Ibrahimovic akiongea na waandishi wa habari alisema
“Mechi hizi za Euro 2016 ndio zitakuwa za mwisho mimi kuichezea Sweden, ni heshima kuwa nahodha wa Sweden kwa kipindi chote, popote nitakapoenda nitakuwa na bendera ya Sweden kwa sababu mimi ni msweden”

No comments

Powered by Blogger.