Gareth Bale avunja rekodi iliyodumu kwa miaka 58 kwenye timu ya taifa
Mchezaji wa Real Madrid, Galeth Bale amefanikiwa kuivunja rekodi ya Ivor Allchurch aliyoiweka miaka 58 kwenye timu ya taifa Wales baada ya kufunga kwenye mechi tatu mfululizo kwenye michuano ya kombe la Euro yanayoendelea huko Ufaransa na kufikisha magoli 23 katika mechi 59 alizocheza mpaka sasa.
Bale alifanikiwa kufunga goli lake la tatu kwenye mashindano hayo walipoifunga timu ya Urusi jumla ya magoli 3-0 kwenye mashindano hayo ya Euro huku akiwa tayari ameshazifunga timu za Slovakia na Uingereza walizokuwa nazo kwenye kundi moja la michuano hiyo.
Bale ameanza michuano ya Uero 2016 akiwa mwenye bahati kubwa ambayo haijawahi kuwatokea wachezsaji wengi tangu walipofanya hivyo kina Milan Baros wa Jamhuri ya Czech na Ruud van Nistelrooy wa Uholanzi waliofunga mechi zote tatu katika Euro 2004.
No comments