Header Ads

Header ADS

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri wapya wa mambo ya ndani na yule wa kilimo siku mbili tu baada ya kutangaza mabadiliko madogo katika baraza lake la mawaziri.

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri wapya wa mambo ya ndani na yule wa kilimo siku mMchembabili tu baada ya kutangaza mabadiliko madogo katika baraza lake la mawaziriWaziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Lameck Nchemba akipeana mkono na Rais Magufuli muda mchache baada ya kuapishwa.
Jumamosi iliyopita Rais Magufuli alitangaza uteuzi wa mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi.
Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, bwana Mwigulu Lameck Nchemba aliteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi.
Kupitia ukurasa wa twitter Mchemba ameandika:

#ASANTE Mh.Rais J.P.Magufuli kwa kuendelea kuniamini na kunipa dhamana ya kuongoza wizara ya mambo ya ndani ya nchi.Bwana Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani bw Charles Muhangwa Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

No comments

Powered by Blogger.