Linah adai hataki tena kufanya makosa kwenye kutafuta label mpya ya kumsimamia
Msanii mahiri wa muziki, Linah Sanga amesema hatafanya tena makosa ya
kusaini mkataba na label yoyote kama alivyofanya makosa katika kipindi
cha nyuma.
Muimbaji huyo ambaye aliwahi kutamba na wimbo ‘Ole Themba’, mara ya mwisho alikuwa chini ya label ya muziki ya ‘Pan Musiq’ ambapo alifanikiwa kufanya project kadhaa ikiwemo ya ‘No Stress’.
Akiongea Jumatatu hii, Linah amesema amechoka kuhamahama katika label.
“Kuna label nyingi sana zinataka kufanya kazi na mimi,” alisema Linah. “Lakini mimi bado siko tayari kwa sababu nimeshapita katika label kama tatu au nne na nimeshaona ugumu uliopo. Sitaki tena kufanya makosa kwa sababu sipendi ile hali ya kuhamahama , kwa hiyo nahitaji label ambayo nitakubaliana nayo kwenye kila kitu,”
Muimbaji huyo ambaye hivi karibuni ameachia video ya wimbo ‘Imani’, amesema kwa sasa anakabiliwa na ukata wa pesa hali ambayo inamfanya ashindwe kuachia kazi zake kwa wakati

No comments