Header Ads

Header ADS

Kitakacho punguza mwili wangu ni stress sio balance diet -Msechu

Msanii wa muziki Peter Msechu amesema mbinu ya kufanya diet ili mwili wake upungue imemshinda hivyo anaamua kujipa stress ambazo zimfanya akonde.msechu
Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumatano hii, Msechu amesema gharama za kufanya diet zimemshinda.
“Mambo ya kusema nafanya diet mimi siwezi hizo hela za kununua matunda ya elfu nne kila siku mimi sina, sijui hela ya gym hamna,” alisema Peter Msech
Aliongeza,”Sasa hivi mimi nataka stress tu ili nipungue maana kitambi hiki saizi kimekuwa na mazalia kama arobaini hivi,” alisema
Hivi karibuni Peter Msechu ameachia wimbo mpya uitwao ‘Mama’, akiwa ameshirikia na Banana Zoro.

No comments

Powered by Blogger.