Usain Bolt kuchuana na Adam Gemili
Bingwa mara mbili wa Olimpiki wa
riadha Usain Bolt amethibitisha kwamba yeye atashiriki katika michezo ya
maadhimisho mjini London umbali wa Mita 200 hapo Julai 22 .
Raia
huyo wa Jamaica mwenye miaka 29 ambaye ana rekodi ya dunia ya kukimbia
mita 200 na sekunde 19 , atakabiliana na Muingereza Adam Gemili.Naye mfukuza upepo Zharnel Hughes, mshindi namba tano wa mwaka jana katika michuano ya Dunia 200m, naye anatarajia kushiriki katika mbio hizo.
No comments