Header Ads

Header ADS

Ibaki Story imeandikwa na mwandishi wa Moyo Mashine ya Ben Pol? Haya ni majibu ya Rich Mavoko

So mtaani kuna tetesi kuwa hit mpya ya Rich Mavoko imeandikwa na mwandishi wa wimbo wa Ben Pol ‘Moyo Mashine’, Lollypop. imageMavoko amezijibu tetesi hizo kupitia 255 ya XXL kupitia Clouds FM na kudai kuwa ni kweli mwandishi huyo amehusika lakini si kama inavyosemwa na si kweli kwamba amekausha kutoa credits.
Amesema Ibaki Story imepita kwenye mikono ya wapishi wengi na pindi alipojiunga na WCB ilifumuliwa na kupangwa upya.
Amemtaja Kevin Snap kuwa ndiye producer aliyeianza kazi hiyo kabla ya kupelekwa kwa Man Walter na kisha kupelekekwa Lollypop aliyeongeza vitu vyake pia.
“Nilipohojiwa kwa mara ya kwanza kabisa nilimtaja [Lollypop] kati ya watu waliopata tabu na hiyo nyimbo lakini alipiga vitu vizuri, Kevin Snap alifanya vitu vizuri kwahiyo ni kazi ambayo ilifanywa na watu wengi,” alisema Mavoko.
Aliwataja maproducer walioigusa kazi hiyo kuwa ni pamoja na Kevin, David, Mazuu, Walter na Lollypop huku final production ikifanywa na Tudd Thomas.
Hata hivyo Mavoko hakueleza iwapo wimbo huo kweli uliandikwa na Lollypop au tu aliishia kuchangia vitu kwenye utayarishaji.https://youtu.be/q6kpPcspWPE

No comments

Powered by Blogger.