Watu weusi hufungwa zaidi bila hatia
Kutambua mshukiwa kwa kutumia picha zinazojaribu kumkisia mhalifu |
Kile ambacho Marvin Anderson alitaka kukifikia katika maisha yake ni kuwa mzima moto. Lakini badala yake katika umri wa miaka 18, akawa ametuhumiwa kwa kubaka, kuteka na kuiba.
Wakati jaji wa Virginia alipotoa hukumu atumikie kifungo cha miaka 210. “Mwili wangu wote ulikufa ganzi,” Anderson amekiambia Kituo cha Televisheni cha CNN. “Nilijua nitafungwa kwa kosa niliokuwa sijalifanya.
Ilinichukua miaka 15 nikiwa jela na miaka mitano ya kuachiwa huru kwa masharti kabla ya kufutiwa hatia—baada ya vipimo vya vinasaba (DNA) kuthibitisha hakuwa na hatia."
“Nilikuwa naamini mfumo wa sheria lakini ukaniangusha,” amesema.
Anderson ni mmoja kati ya mamia ya watu weusi ambao wamehukumiwa na baadae kuachiliwa huru kwa makosa waliokuwa hawajafanya.
Ripoti mpya iliyotolewa na Masjala ya Kitaifa ya Watu waliofutiwa hatia (NRE), mradi wa pamoja kati ya Chuo Kikuu cha California, Irvine: Chuo Kikuu cha Michigan- Shule ya Sheria na Chuo Kikuu cha Jimbo-Shule ya Sheria , inaonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa watu weusi kutuhumiwa na kufungwa bila ya makosa kuliko watu weupe na pia wanaweza kukaa jela muda mrefu kabla ya kujulikana hawana hatia.
Wakati watu weusi wanawakilisha asilimia 13 ya idadi ya wananchi wa Marekani, lakini wana idadi kubwa ya watu waliofutiwa hatia katika daftari la masijala la Taifa.
Katika baadhi ya matukio, unaona wazi aina fulani ya ubaguzi,” amesema Samuel Gross, Profesa wa Sheria, Chuo Kikuu cha Michigan. Yeye pia ni mhariri wa ngazi ya juu wa ripoti hiyo. Ubaguzi usiowazi pia ni sababu inayopelekea hilo, Gross amesema.
Watafiti hao wamejikita katika vitu vitatu katika makosa ya jinai ambapo watu weusi wanauwezekano mkubwa kuliko watu weupe kutuhumiwa kwa makosa ambayo hawajafanya: kuuwa, kubaka na makosa ya madawa. Wakati wakikiri kuwa sababu zinazopelekea kusingiziwa makosa wasio yafanya “zina tofautiana kwa kiwango kikubwa kati ya kosa moja hadi jingine,” Pia wanasema wamekuta aina za ubaguzi wa rangi katika makundi yote matatu yaliyohusishwa na tafiti hiyo.
Kwa mujibu watafiti, watu weusi wasio na makosa wana uwezekano mara saba zaidi kutuhumiwa kwa mauaji kuliko watu weupe. Gross amesema kwa namna fulani asilimia za kesi za mauaji kati ya watu weusi ziko juu zaidi kuliko miongoni mwa watu weupe, na hivyo watu weusi wasiokuwa na makosa wanauwezekano mkubwa wa kudhaniwa wametenda makosa na kufungwa kwa mauaji.
Zaidi ya hilo, kesi za mauaji ambako mtuhumiwa mweusi amehukumiwa kwa makosa ziko takriban asilimia 22 na inawezekana zikahusisha uvunjifu wa sheria kwa upande wa polisi kuliko wale watu weupe waliotuhumiwa.
Gross amesema watu weupe sio mara nyingi wanaweza kutambua nyuso za watu weusi—nadharia ya “upendeleo wa rangi yako” katika mchanganyiko wa kutambua rangi mchanganyiko.
Inapokuja katika makosa ya jinai ya dawa, watu weusi wanauwezekano mara 12 zaidi kufungwa kuliko watu weupe katika makosa hayo. Wakati makundi ya watu weusi na weupe wanaviwango sawa katika utumiaji wa dawa haramu, watu weusi wanauwezekano mkubwa kukamatwa na kufungwa kwa makosa haya kuliko watu weupe, watafiti wamegundua hilo.
No comments