Header Ads

Header ADS

MWANAMUZIKI VANESSA MDEE AKAMATWA NA POLISI KWA DAWA ZA KULEVYA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia mwanamuziki Vanessa Mdee maarufu Vee Money kwa tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.


Akizunguzumzia taarifa hiyo, Mwanasheria wa mwanamuziki huyo, Amin Tenga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa Vanessa alijisalimisha mwenyewe katika kituo cha polisi kama alivyoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati akitaja majina ya watuhumiwa wa dawa hizo mapema mwezi uliopita.


Vanessa ni miongoni mwa watu waliotajwa katika orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya, lakini hakuweza kuripoti kwa wakati sababu alikuwa nchini Afrika Kusini kikazi.


Baada ya kujisalimisha, Jeshi la Polisi lilifanya upekuzi nyumbani kwake kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.


Jeshi la Polisi hadi sasa halijatoa taarifa kuhusu tukio hilo na kama walikuta ushahidi wowote nyumbani kwa mwanamuziki huyo.


No comments

Powered by Blogger.