TIZAMA-Rapper wa Kenya Femi One awataja wasanii wa Bongo anaotamani kufanya nao kazi
Rapper wa kike kutoka Kenya, Femi One amewataja wasanii wa Bongo Flava ambao anatamani kufanya nao kazi.
Femi amewataja wasanii hao kuwa ni pamoja na G-Nako, Joh Makini na Ruby.
“Napenda kufanya kazi na Joh Makini kutokana na anavyochana, Gnako anavyoflow kwa style nyingi. Msanii mwingine ni Ruby, naipenda sauti yake lakini pia nampenda Nay wa Mitego alivyokuwa haogopi kutaja watu kwenye nyimbo zake,” amesema Femi.
Mpaka sasa rapper huyo ameshaachia video mbili ikiwemo ‘Jah’ na yupo chini ya lebo ya Kaka Empire inayomilikiwa na King Kaka.
No comments