TIZAMA-Mshindi wa Maisha Plus apanga kuingia kwenye filamu
Safari moja huanzisha nyingine. Mshindi wa shindano la Maisha Plus, Olivie Kiarie wa Kenya amefunguka jinsi atakavyozitumia fedha alizoshinda kwenye shindano hilo.
Akiongea na gazeti la Mtanzania, Olivie amesema kuwa atatumia fedha hizo kujifunza taaluma ya uandaaji wa filamu. Ameongeza kuwa, “Nilipanga kutoa fungu la 10 la fedha nitakazoshinda kwa watoto yatima nyumbani kwetu, hilo lazima nilitimize.
Ushindi huo ulimpatia Olivie kitita cha shilingi milioni 30 za kitanzania. Shindano hilo lilishirikisha nchi za Afrika Mashariki.
No comments