TIZAMA | Afrima Awards: Diamond Platnumz aondoka na tuzo tatu (Picha/Video)
Diamond Platnumz ameibuka na ushindi wa nguvu kwenye tuzo za Afrima 2016 zilizotolewa Jumapili hii jijini Lagos, Nigeria. Muimbaji huyo ameshinda tuzo tatu, Song of The Year – Utanipenda, Best Artist/Duo/Song Of The Year Utanipenda na Best Male Artist in Eastern Africa.
Diamond akishukuru baada ya kushinda tuzo ya tatu kwenye Afrima Pamoja na ushindi huo, Diamond pia alitumbuiza wimbo alioimba na Papa Wemba, msanii aliyetunukiwa tuzo ya heshima. |
No comments