Dully Sykes awataja wasanii watatu aliowasaidia na leo wanalipa fadhila
Msanii mkongwe katika muziki wa Bongo Flava, Dully Skyes amesema katika wasanii wote ambao aliwahi kuwasaidia kimuziki mpaka wakafanikiwa, ni watatu tu ndio ambao wamekuwa wakilipa fadhila kwake na ambao wamekuwa wakimpigania.
Dully Skyes alisema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo na kudai amewasaidia wasanii wengi lakini wengi wao wanaishia kumuita tu ‘brother’ lakini si Diamond Platnumz, Mr Blue na Queen Darlin.
“Watu ambao nimewasaidia wananipa heshima ni wawili tu, wengine wanaishia kuniita brother D tu, lakini Diamond Platnumz, Mr Blue pamoja na Queen Darlin ndiyo wananipa ile heshima kabisa na wana uchungu na mimi kwamba huyu kaka yetu. Kwahiyo katika wale watoto ambao nimewatoa kwenye muziki wakiwa wadogo na wananisaidia ni hao watatu,” alisema.
Hivi karibuni Diamond kupitia label ya WCB alimpa ofa Dully ya kughramia mradi mzima wa wimbo wake unaoendelea kufanya vizuri, Inde akiwa na Harmonize
No comments