Albamu ya Stamina ‘Mt Uluguru’ imeingiza Tsh milioni 45
Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Morogoro, Stamina amesema tayari ameshafunga mahesebu ya mauzo ya albamu yake ya ‘Mt Uluguru’ ambayo aliisambaza nchini nzima.
Rapper huyo akiongea mpaka anafunga duka la kuuza albamu hiyo tayari alishauza nakala 9,000 kwa bei ya tsh 5000 na chache kwa tsh 10,000.
“Niliuza nakala 9,000,” alisema Stamina. “Kilicho nisaidia ni uzinduzi wangu wa Morogoro, pia ni washukuru mawakala wangu kutoka katika vyuo mbalimbali nchini, kwa sababu wao walikuwa wanachukua mzigo alafu baadaye wananitumia mauzo na kusema kweli biashara ilikuwa nzuri,”
Mapema mwaka huu rapper huyo aliachia albamu hiyo na kuizindua kwa show kubwa ambayo ilifanyika Morogoro na kusindikiza na mastaa kibao wa muziki.
No comments