Waumini wampinga Askofu waingia kanisani na Mabango
Waumimi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki, Kanisa Kuu la Mtwara wameingia katika ibada na mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali wa kumpinga Askofu Mkuu wa dayosisi hiyo, Lucas Mbedule kwa tuhuma za kukiuka katiba, unyanyasaji wa watumishi na ubadhilifu wa fedha za ushirika na dayosisi.
Hata hivyo, Askofu Mbedule amesema asingependa kuyazungumzia suala hilo kwa sababu walikaa kikao.
Umoja wa wazee ulitoa tamko ndani ya kanisa hilo kutokana na tuhuma zinazomkabili askofu huyo na kumtaka asijihusishe na mambo yanayohusu usharika na dayosisi, ili kupisha uchunguzi na kumwomba Mkuu wa KKKT, Dk Fredrick Shoo kuunda tume kuchunguza tuhuma hizo.
Akisoma tamko la wazee wa kanisa hilo, Amon Mkocha amesema wanapinga uamuzi uliofanywa na kikao cha halmashauri kuu kilichofanyika mwezi huu
No comments