Nay wa Mitego kuja na kolabo ya remix ya wimbo ‘Pale Kati’ akiwa na msanii wa Kimataifa
Rapper Nay wa Mitego amefunguka kwa kusema kuwa tayari ameshawatumia beat baadhi ya wasanii wa Kimataifa ambao waliomba kuwepo kwenye remix yake ya wimbo ‘Pale Kati’
Akiongea Jumatatu hii, Nay amesema ni mapema kuweka wazi ni msanii gani atashiriki kwenye remix hiyo.
“Remix inakuja, tayari kuna wasanii wawili watatu ambao waliomba kushiriki na tayari nimeshawatumia, kwa hiyo ninachosubiria ni kuangalia nani amekaza alafu ndo nitangaze nimefanya na nani,” alisema Nay. “Lakini ni wasanii wakubwa, tena mmoja na yule ambaye nilitangaza kufanya naye kolabo ambayo bado haijatoka na hiyo ipo tayari, sema baada ya kuisikia hii kazi akaomba tufanye remix,”
Wimbo huo ambao ulifungiwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kutoka na kigezo cha maadili, unadaiwa kufanya vizuri katika nchi za jirani hasahasa Kenya, Uganda pamoja na Burundi.
No comments