Mchezaji akataa kuheshimu wimbo wa taifa Marekani
Mchezaji wa soka ya Marekani NFL amekataa kusimama ili kutoa heshima wakati ambapo wimbo wa taifa unapoimbwa akipinga kile anachotaja ni ubaguzi wa rangi.
Colin Kaepernick ,anayeichezea timu ya San Fransisco 49ers alisalia akiwa ameketi wakati wimbo wa taifa ulipoimbwa.
''Sitasimama kujivunia bendera ya taifa linalokandamiza watu weusi na watu wengine wa rangi'',alielezea.
Mashabiki wengine walimzoma ,mchezaji huyo wakati alipoingia uwanjani.
Lakini timu yake imesema kuwa inaheshimu haki yake ya kugoma wakati timu ya 49ers ilipokuwa ikikabiliana na Green Bay Packers katika mechi ya kirafiki.
''Tunatambua uhuru wa mtu binafsi kujichagulia na kushiriki katika sherehe za wimbo wa taifa'',timu hiyo ilisema. akipinga kile anachotaja ni ubaguzi wa rangi
No comments