Droo Europa League: Man Utd kukutana na Robin van Persie
Manchester United watakutana na klabu anayochezea nyota wao wa zamani Robin Van Persie- Fenerbahce- pamoja na Feyenoord na Zorya Luhansk hatua ya makundi Europa League.
Klabu ya KRC Genk anayochezea Mtanzania Mbwana Ally Samatta imewekwa kundi F na Athletic Bilbao ya Uhispania, Rapid Vienna ya Austria na Unione Sportiva Sassuolo Calcio kwa ufupi Sassuolo ya Italia
Southampton, klabu nyingine ya Ligi ya England inayocheza michuano hiyo, imepangwa kucheza dhidi ya Inter Milan, Sparta Prague na Hapoel Beer Sheva.
Dundalk ya Ireland nayo imepangwa na h Zenit St Petersburg, AZ Alkmaar na Maccabi Tel-Aviv baada ya droo kufanywa Monaco
Meneja wa United Jose Mourinho amesema hawafahamu vyema wapinzani wao Zorya, kutoka Ukraine, lakini amefurahia kuwekwa kundi moja na Fenerbahce na Feyenoord.
"Sote twafahamu kwamba shindano hili si kama Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya lakini kuwa na Manchester United ikikutana na klabu zenye historia ndefu kama vile Fenerbahce na Feyenoord ni jambo zuri kwetu," amesema.
Droo kamili:
Kundi A: Man Utd, Fenerbahce, Feyenoord, Zorya Luhansk
Kundi B: Olympiacos, Apoel Nicosia, Young Boys, Astana
Kundi C: Anderlecht, St Etienne, Mainz, Qabala
Kundi D: Zenit St Petersburg, AZ Alkmaar, Maccabi Tel-Aviv, Dundalk
Kundi E: Plzen, Roma, Austria Vienna, FC Astra Giurgiu
Kundi F: Athletic Bilbao, Genk, Rapid Vienna, Sassuolo
Kundi G: Ajax, Standard Liege, Celta Vigo, Panathinaikos
Kundi H: Shakhtar Donetsk, Braga, Gent, Konyaspor
Kundi I: Schalke 04, FC Red Bull Salzburg, Krasnodar, Nice
Kundi J: Fiorentina, PAOK Salonika, Liberec, Qarabag
Kundi K: Inter Milan, Sparta Prague, Southampton, Hapoel Beer Sheva
Kundi L: Villarreal, Steaua Bucharest, FC Zurich, Osmanlispor
No comments