Dereva maarufu wa mbio za magari wa nchini Afrika Kusini, Gugu Zulu amefariki dunia wakati akipanda Mlima Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.Kifo chake kimethibitishwa na taasisi ya Nelson Mandela iliyokuwa imeandaa upandaji huo wa mlima Kilimanjaro ujulikanao kwa jina la Trek4Mandela. Zulu alikuwa sehemu ya kundi la waafrika Kusini wengine waliokuwa wakipanda mlima huo akiwemo mke wake, Letshego Zulu.Taasisi hiyo imedai kuwa Zulu amefariki Jumatatu hii wakati akijaribu kufika kwenye kilele cha mlima huo. Inadaiwa kuwa Gugu alipata shida ya kupumua na watu wa huduma ya dharura walimwekea drip na kushuka naye
No comments