WADA yaishutumu Urusi
Shirika
linalopambana na matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku
michezoni,WADA, limeishutumu Urusi kwa kuendelea kukwamisha jitihada
zake za kufanya vipimo kwa wanariadha.
WADA imesema, katika
kipindi cha miezi sita tangu mwezi Novemba mwaka jana, watu wanaofanya
vipimo wamekuwa wakipata vitisho mara kwa mara kutoka kwa askari wa
usalama.Kwa mujibu wa Ripoti yake, maafisa wake wamekuwa wakipata ugumu kuingia kwenye miji ya kijeshi nchini Urusi .Ripoti imedai kuwa wamekuwa wakiwekewa vikwazo vya makusudi ili kukwamisha programu na pia wamekuwa wakifuatiliwa na vikosi vya usalama wanapokuwa wanatimiza majukumu yao.
Pia Sampuli zinazofanyiwa vipimo zimedaiwa kuchezewa.
Ripoti ya WADA imekuja siku mbili kabla chama cha riadha duniani, kuamua kuhusu mustakabali wa washindani kushiriki michuano ya Olimpiki ya Rio Brazil mwezi Agosti au la.
Mwezi Novemba mwaka jana, wanariadha wa Urusi walipigwa marufuku kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kubaini wachezaji kujihusisha na matumizi ya dawa za kusisimua misuli.
WADA imesema taarifa yake imefikishwa kwenye Chama cha riadha duniani
No comments