Header Ads

Header ADS

Europa:Uingereza yaibomoa Wales


Wachezaji Jamie Vardy na Daniel Sturridge wameitoa kimaso maso Uingereza kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Wales kwenye Mechi ya Kundi B na kuwapaisha hadi kileleni mwa Kundi hilo.
Wales walitangulia kuzitikisa nyavu za Uingereza kwa bao la Gareth Bale na baadaye Uingereza wakasawazisha bao hilo na kuongeza bao la pili la ushindi.
Ushindi huu umewaweka Uingereza kileleni na kufikisha alama 4 wakifuatiwa Wailes na Slovakia zenye alama 3 kila mmoja, huku Urusi ikiburuta mkia kwa alama 1.
Wales ambao kuifunga uingereza tangu 1984 waliposhinda 1-0 kwa Bao la Mark Hughes, ambae sasa ni Meneja Stoke City, alipocheza Mechi yake ya kwanza kwa Wales, walitangulia kuifunga uingereza kwa Frikiki ya Dakika ya 42 iliyopigwa na Gareth Bale umbali wa Mita 30 na Kipa Joe Hart kufanya makosa.

No comments

Powered by Blogger.