Batuli azungumzia kurejea kwa tamthilia za mastaa wa Bongo, atoa ushauri huu
Muigizaji wa filamu nchini, Yobnesh Yussuf maarufu kama Batuli amesema
yeye ni mmoja wa watu waliofurahi kuona kuwa waigizaji maarufu nchini
wanarejea kwenye tamthilia. Miongoni mwa waigizaji wanaokuja na tamthilia zao ni JB, Irene Uwoya
pamoja na Ray na Johari. Amesema kwa ulimwengu wa sasa tamthilia
haziepukiki na ni muhimu Tanzania zikawepo nyingi pia.
No comments