Header Ads

Header ADS

Alawi Junior amvuta Christian Bella, aeleza kwanini nyimbo zake nyingi ni kolabo

Msanii wa muziki, Alawi Junior anajipanga kuachia kazi yake mpya akiwa amemshirikisha mkali wa masauti Christian Bella.
Muimbaji huyo ambaye tayari ameshafanya kolabo kadhaa na baadhi ya mastaa wa muziki, akiongea Jumatatu hii kuwa anapenda kufanya kolabo ili kuchanganya ladha katika muziki wake.
“Muziki ni kazi kama kazi nyingine, ubunifu ni kitu muhimu sana, kwa hiyo mimi ngoma zangu nyingi niza kolabo kwa sababu napenda kuchanganya ladha ya muziki, kama nafasi ninayo kwanini nisifanye,” alisema Alawi.
Aliongeza, “Na bado nitaendelea kufanya kolabo. Tayari nina kazi na Christian Bella, itatoka hivi karibuni audio na video, kwa hiyo mimi naamini kila msanii ana mashabiki wake,”
Muimbaji huyo tayari ameshafanya kolabo kadhaa na mastaa wa bongo, akiwemo Barnaba ya wimbo Bado pamoja na Rich Mavoko ya wimbo ‘Love Matata’.
Alawi Junior

No comments

Powered by Blogger.