Serikali yashauriwa kupiga marufuku viroba
Mkurugenzi wa kituo cha wagonjwa wasiojiweza cha Bashay wilayani Mbulu, Mkoa wa Manyara, Padri James Amnaay alitoa rai hiyo juzi alipopokea msaada wa vyakula, nguo na sabuni kutoka Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wilayani hapa.
Padri Amnaay alisema iwapo Serikali itapiga marufuku pombe hizo, itasaidia vijana kutojiingiza kwenye ulevi ambao umekithiri na kusababisha baadhi yao kuwa vichaa.
Alisema kutokana na urahisi wa kubeba na bei nafuu, pombe hizo zimewaathiri vijana wengi wanaokunywa na kulewa hatimaye kujiingiza kwenye dawa za kulevya
No comments