Mwanasheria wa Wema na Vanessa Albert Msando afunguka kuhusu tuhuma zinazowakabili wawili hao
Mwanasheria wa Wema Sepetu pamoja na Vanessa Mdee, Albert Msando amefunguka na kuzungumzia nini kinaendelea kwa wateja wake wawili hao ambao wanakabiliwa na tuhuma za kuhusika na biashara ya Madawa ya kulevya.
Wawili hao ni miongoni mwa wasanii waliotajwa katika list ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuwa wanatuhumiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya.
Wema bado anaendelea kushikiliwa na jeshi lilo huku Vanessa Mdee ambaye alitajwa katika list ya pili ya RC Makonda na kutakiwa kuripoti kituoni hapo Jumatatu hii yupo Afrika Kusini na leo amewakilishwa na mwanasheria wake Albert Msando.
Mama Wema akiwa kituoni hapo
Akiongea Jumatatu hii, Albert Msando amesema kwa upande wa Wema bado jeshi la polisi linaendelea na upelelezi na pindi litakapokamilisha ataeleza nini kinaendelea.
“Mimi nipo hapa kwajili ya Wema Sepetu na Vanessa Mdee,” alisema Albert Msando. “Kwa Wema bado upelelezi unaendelea, kesho baada ya upelelezi kukamilika tutajua anapelekwa mahakamani au la,”
Kwa upande wa Vanessa Mdee mwanasheria huyo alidai muimbaji huyo wa wimbo Cash Madame bado yupo Afrika Kusini na leo amemwakilisha.
Wasanii wengine ambao bado wanashikiliwa na jeshi hilo ni TID, Nyandu Tozzy pamoja na Recho na Tunda ambao wamefika leo kituoni hapo.
No comments