Mimi siwezi kuoa kwa sababu fulani kaoa – Chege
Msanii mkongwe wa muziki Chege Chigunda amedai hawezi kufuata mkumbo kuoa kwa sababu fulani kaoa
Chege akiwa na Nandy |
Muimbaji huyo ambaye hivi karibuni ameachia wimbo mpya “Kelele za Chura” akiwa amemshirikisha Nandy, amedai suala la kuana linakuja kutoka kwa Mungu na sio kuigana.
“Mimi siwezi kuoa sijui kwa sababu nikienda kwenye interview nitaulizwa, mbona wewe haujaoa, mbona mwenzako kaoa, na siwezi kuoa kwa sababu Mh Temba kaoa,” Chege aliiambia Global TV. “Mimi nitaoa pindi tu mwenyezi Mungu atakaposema Chege oa lakini sio kwa sababu fulani kafanya hivyo,”
Muimbaji huyo ni msanii pekee wa Kundi la TMK Wanaume Halisi ambaye bado anafanya vizuri katika muziki.
No comments