Stereo– Ninatamani sana nimuoe Chemical
Rapper Stereo amedai kuwa anatamani rapper Chemical aje kuwa mke wake wa ndoa
Stereo amesema Chemical ambaye jina lake halisi ni Claudia Lubao ni msichana anayemzimia kupita maelezo. Ameamua kufungua moyo wake kwenye mahojiano na mtangazaji wa CG FM ya Tabora, Manoni MJ wa Pili.
“Nadhani tukioana tutakuwa na familia hivi ya aina yake,” alisema Stereo na kuongeza kuwa bado hajamweleza Chemical takwa la moyo wake.
“Mimi nampenda Chemical kuliko mnavyofikiria,” amesisitiza rapper huyo.
No comments