Header Ads

Header ADS

Muziki ya Darasa yafikisha views milion moja ndani ya wiki mbili

Uamuzi wa kubadilisha muziki wake, umeendelea kumzalia matunda matamu rapper Darassa. Akiwa na wimbo ambao hakuna anayeweza kubisha kuwa ndio namba moja nchini kwa sasa, Muziki, mkali huyo kajiandikia rekodi yake nyingine katika CV yake
Video ya wimbo wake huo imefikisha zaidi ya views milioni 1 ndani ya wiki mbili tangu iwekwe kwenye mtandao wa Youtube. Ni nadra sana kwa msanii anayerap kufikisha idadi hiyo ya views katika kipindi hicho.

Wimbo huo kwa muda mfupi umemfanya Darassa awe miongoni mwa wasanii wanaotafutwa sana kwa show wakati huu.

No comments

Powered by Blogger.