Header Ads

Header ADS

Mourinho atoa neno kuhusu kuumia kwa Maktaryan

Kiungo wa Manchester United na timu ya Taifa ya Armenia Henrikh Mkhitaryan baada ya kuumia katika mechi dhidi ya Tottenham, kwa kukwaana na mchezaji Danny Rose hali iliyopelekea kuondolewa uwan

jani akiwa kwenye machela dakika ya 85, na mashabiki wamekuwa na wasiwasi kuhusu jeraha lake
                  
Kocha wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amewatoa hofu mashabiki wa klabu hiyo kwa kuwaeleza kuwa mchezaji huyo atakuwa nje kwa muda wa wiki moja pekee.
Meneja wa United Jose Mourinho hata hivyo alisema jeraha hilo si mbaya sana.
“Inaonekana kama atakosa mechi kadha zijazo, lakini hatahitaji upasuaji. Twatumai atarejea siku ya Boxing Day,” Mourinho aliambia MUTV.
Mourinho alikuwa awali ameeleza wasiwasi kwamba jeraha hilo lingekuwa mbaya lakini baadaye akasema watamkosa kwa “wiki kadha tu”.
Atakosa mechi ya Jumatano ugenini dhidi ya Crystal Palace na mechi ya Jumamosi dhidi ya West Bromwich Albion. Huenda akarejea kucheza dhidi ya Sunderland mnamo 26 Desemba.
Mkhitaryan ambaye alifunga bao pekee ambalo lilihakikisha ushindi wa Manchester United dhidi ya Tottenham kwenye uwanja wa Old Trafford kabla ya kuumia na kutolewa nje.

No comments

Powered by Blogger.