Header Ads

Header ADS

Adhabu ya FA kwa Jose Mourinho

Moja kati ya habari zilizoingia kwenye headlines leo November 30 2016 ni kuhusiana na kocha wa Man United Jose Mourinho ambapo chama cha soka England FA kimetangaza kumfungia mechi moja kukaa katika benchi na kumpiga faini ya pound 16,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 40 kwa utovu wa nidhamu.
Mourinho amepewa adhabu hiyo kutokana na kosa la kupiga chupa ya maji kwa hasira wakati wa mchezo wa Man United dhidi ya West Ham United uliomalizika kwa sare ya goli 1-1, Mourinho alipiga chupa hiyo baada ya refa Jon Moss kumuonesha kadi ya njano Paul Pogba kwa kujianguasha.
Kama utakuwa unakumbuka Jose Mourinho hilo litakuwa kosa la pili kulifanya ndani ya mwezi mmoja, baada ya October 29 kutolewa katika benchi katika mchezo dhidi ya Burnley na baadae  FA ikampiga faini ya pound 8,000 na kufungiwa mechi moja kukaa katika benchi



No comments

Powered by Blogger.