Video: Bondia afariki dunia baada ya kupokea kichapo ulingoni
Bondia Mike Towell (25) amefariki dunia baada ya kupoteza pambano lake na Dale Evans kwenye mzunguko wa tano. Pambano hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa St Andrews Sporting Club Alhamisi iliyopita. Baada ya kupoteza pambano hilo hali yake ilibadilika na kukimbizwa hospitali ambako baadaye alifariki dunia.
Ripoti ya madaktari imeonesha kifo cha Mike kimesababishwa na kuvujiwa na damu nyingi kwenye ubongo baada ya fuvu lake kupata madhara.
Kabla ya kupoteza pambano hilo bondia huyo aliangushwa mara mbili kwenye mzunguko wa kwanza kabla ya kuangushwa tena kwa konde zito na kushindwa kuendelea na pambano
No comments