Header Ads

Header ADS

Man United yapoteza mechi kwa mara ya tatu mfululizo

Klabu ya Manchester United imepoteza mechi kwa mara ya tatu mfululizo katika kipindi cha juma moja baada ya kufungwa tena na klabu ya Watford kwa magogoli 3-1 .
Watford walikuwa wa kwanza kupata goli lilifungwa na Daryl Janmaat kabla ya Marcus Rashford kusawazisha.
Lakini mchezaji wa ziada Zuniga alifunga ikiwa imesalia dakika saba mchezo kukamilika.

Deeney baadaye alifunga penalti katika mda wa ziada baada ya Marouane Fellaini kumchezea vibaya katika eneo la hatari.
Hii ni mara ya tatu mfulilozi kwa Manchester United kupoteza,ikishindwa 2-1 na Manchester City,baadaye ikapoteza 1-0 dhidi ya klabu ya feyenoord ya Uholanzi katikati ya wiki katika kombe la bara Ulaya


No comments

Powered by Blogger.