Header Ads

Header ADS

Video: Goli la kwanza la Samatta kwenye msimu mpya wa ligi ya Ubelgiji

Nyota ya nahodha wa timu ya Taifa Stars, Mbwana Samatta imezidi kung’aa ndani ya Belgium Pro League
          Mchezaji huyo alifanikiwa kuifungia timu yake ya RC Genk bao la pili kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KV Oostende akitokea benchi dakika 10 kabla ya mechi kumalizika.

Nikolaos Karelis alianza kuifungia Genk goli la kuongoza dakika ya 50, kwenye dakika ya kwanza ya nyongeza za refa, Mbwana Samatta aliipatia Genk bao la pili lakini dakika mbili baadaye mchezaji raia wa Zimbabwe, Knowledge Musona aliifungia KV Oostende bao la kufutia machozi. 
    

No comments

Powered by Blogger.