Roberto Martinez: Kocha wa zamani Everton apewa kazi Ubelgiji
Meneja wa zamani wa Everton, Wigan na Swansea Roberto Martinez ameteuliwa mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya Ubelgiji.
Martinez, 43, ambaye ni raia wa Uhispania, alifutwa kazi Everton mwezi Mei baada ya kufanya kazi Goodison Park kwa miaka mitatu.
Marc Wilmots alijiuzulu wadhifa wake kama meneja wa Ubelgiji mwezi jana, wiki mbili baada ya kushindwa na Wales robofainali michuano ya Euro 2016.
Nafasi yake ilitangazwa wazi mtandaoni na Shirikisho la Soka la Ubelgiji.
Shirikisho hilo lilisema linamtafuta mtu bingwa katika mawasiliano na mwenye uwazi na ambaye amethibitisha uzoefu katika kuwapa wachezaji nyota ujuzi na ustadi katika ufundi.
No comments