Moyes awataka mashabiki wa Sunderland wasitarajie makubwa kwa kipindi hiki
Kocha mpya wa klabu ya Sunderland David Moyes amewaambia mashabiki wa klabu hiyo kujitayarisha kwa makabiliano ya kushushwa daraja msimu huu baada ya kushindwa mabao mawili kwa moja na Middlesbrough siku ya Jumapili.
Paka hao weusi wamepoteza mechi zao mbili za kwanza chini ya meneja Moyes ambaye alichukua nafasi ya Sam Allardyce ambaye ni meneja mpya wa England msimu huu.
Moyes aliongeza: ‘Sidhani naweza kuficha ukweli. Watu watabaki hoi kwa sababu wanamatumaini kwamba kila kitu kitabadilika kimiujiza-haiwezi kubadilika na haitabadilika.’
Klabu ya Sunderland katika misimu minne wamemaliza katika nafasi ya 17, 14, 16 na 17 mtawalia.
Kampeini za mwaka 2010-11 ndio mara ya mwisho ambapo klabu hiyo haikubadilisha meneja katika msimu huo.
Meneja Steve Bruce, Martin O’Neill, Paolo di Canio, Gus Poyet, Dick Advocaat na Allardyce wote wamewajibika kwa klabu hiyo kwa misimu mitano iliyopita.
No comments