Mabasi ya mikoani kusimamisha huduma Jumatatu
Kuanzia Jumatatu wiki ijayo hakutakuwa na usafiri wa mabasi nchi nzima, baada ya Wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani (Taboa) kuamua kusimamisha huduma hiyo ili yafanyiwe ukaguzi na Polisi
Katibu Mkuu wa Taboa, Enea Mrutu amesema zaidi ya mabasi 4,000 yanayohudumia safari za mikoani, yatasimamisha huduma kuruhusu ukaguzi uliolenga kupunguza ajali za barabarani na kwamba, wameshaiandikia Sumatra barua kuitaarifu juu ya suala hilo.
“Tunataka mabasi yetu yakaguliwe kwa pamoja ili mamlaka husika zithibitishe ubora na kama yanaweza kuendelea kutoa huduma za usafiri bila wasiwasi wowote,” amesema.
No comments