Lionel Messi arejea timu ya taifa ya Argentina baada ya kutafakari
Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi, ametangaza kuwa atarejea katika kikosi cha timu ya taifa ya ArgentinaAugust 12 2016 chama cha soka cha Argentina AFA kimetangaza Lionel Messi amebadili maamuzi yake na kuwa ataendelea kuichezea timu ya taifa ya Argentina.
Messi,29,alitangaza kustaafu kuichezea timu hiyo Julai Mwaka huu kufuatia kukosa penati dhidi ya Chile katika fainali ya michuano ya Copa America Centenario na hivyo taifa hilo kupoteza fainali 3 mfululizo.
.
‘Nimeona kuna matatizo mengi katika soka la Argentina na sitaki kuongeza zaidi, sitaki kusababisha maumivu , lengo langu ni kusaidia katika njia niwezayo’ amesema mchezaji huyo ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara 5.

Nyota huyo ambaye ndiye mfungaji wa muda wote wa Argentina akiwa na magoli 55 katika mechi 113, Septemba mwaka huu atakuwepo katika kikosi cha kocha mpya Edgardo Bauza kitachocheza mechi za kufuzu kombe la dunia 2018 Russia
No comments