Leroy Sane ajiunga na Man City kwa pauni 37m
Chipukizi kiungo cha kati wa Ujerumani Leroy Sane amekamilisha uhamisho kwenda Manchester City kwa gharama ya pauni milioni £37m.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 ametia sahihi kandarasi ya miaka 5 baada ya kutokea Schalke O4.
Meneja mpya wa Man City Pep Guardiola amemmiminia sifa kedekede kiungo huyo akisema kuwa ana kasi na kipaji cha kipekee.
'' ninaamini kuwa jinsi anavyocheza huyo kijana inaonesha wazi kuwa anatalanta ya kuvutia sana , ninatarajia mashabiki wetu watavutiwa na hulka yake''
Sane, aliisaidia Ujerumani kutinga nusu fainali ya mchuano wa Euro 2016, aliifunga klabu yake ya Schalke mabao 33 katika ligi kuu ya Ujerumani.
Schalke ilimaliza msimu katika nafasi ya 5.
''ukimtizama akicheza unavutia na ueledi wake , yaani hababaishwi na mpira wala hasuisui hata anapopewa mpira katika mazingira magumu'' alisema Guardiola.
''Hivi unavyomuona ana umri wa miaka 20 tu lakini tayari ameshajishindia nafasi katika timu ya taifa ,hiyo inatudhihirishia kuwa anakipaji kinachohitaji kunolewa kisha anawiri kitaaluma''
Kwa upande wake Sane amesema kuwa moja ya sababu kuu yake ya kujiunga na Man City ni kupata nafasi ya kujifua chini ya ukufunzi wake Guardiola.
" Wakati huu katika taaluma yangu hii bila shaka Guardiola ndiye kocha ambaye ninahakika atanifaa zaidi na kunikuza'' alisema Sane.
''Sitarajii kupewa nafasi moja kwa moja ila najua baada ya muda nitapata nafasi''
No comments