EFM waja na msimu mpya wa tamasha la Muziki Mnene wakiwa na Vodacom
Kituo cha redio cha EFM, kimetangaza kuja na msimu mpya wa tamasha lake la kila mwaka linalojulikana kama Muziki Mnene litakalozinduliwa Jumamosi, August 27.
General Manager wa EFM, Dennis Ssebo (katikati) akiongea na waandishi wa habari. Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano cha Vodacom, Nandi Mwiyombella
Tamasha hilo mwaka huu litafanyika kwa wiki 12 ambapo muziki utapigwa katika baa 12 jijini Dar na mkoa wa Pwani ambapo mwaka huu kauli mbiu yake ni ‘Tunasepa na Kijiji.’
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jumatatu hii, General Manager wa kituo hicho cha redio, Dennis Ssebo alisema kauli mbiu ya ‘Tunasema na Kijiji’ inamaanisha kuwa kila wiki EFM itaweka kambi kwenye eneo moja kwa muda wa siku nne.
Amedai kuwa vipindi kadhaa vitaruka live kwenye maeneo hayo vikiwemo Joto la Asubuhi, Sports Headquarters, Uhondo na Funga Mtaa. Alidai kuwa pia kipindi cha Funga Mtaa kitatumika pia kusaka vipaji vya waimbaji wa muziki wa Singeli.
Pia Ssebo aliwashukuru Vodacom kwa kuungana nao tena kwenye tamasha hilo kwa mara nyingine.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano cha Vodacom, Nandi Mwiyombella, alisema kampuni hiyo imefurahi kushirikishwa kwenye tamasha hilo. Alidai kuwa tamasha hilo litatumika kuwafikia wateja wake ikiwa ni pamoja na kuwapa burudani.
“Sisi kama Vodacom tumejipanga, watu wajitokeze kwa wingi, tutakuwa tuko pale on ground na bidhaa zetu mbalimbali, simu za mkononi zitakuwepo, tutafanya promotion za bidhaa zetu za kimawasiliano,” alisema Nandi
No comments