Diamond: Muziki si kitu cha lazima kwangu
Diamond amesema kuwa hategemei muziki kuendesha maisha yake
Hit maker huyo wa wimbo wa ‘Kidogo’ hivi karibuni kupitia kipindi maalum cha kituo cha runinga cha E!TV, E Vip aliutaja utajiri wake kuwa ni dola milioni 4 za Kimarekani ambao kwa shilingi ya Tanzania ni zaidi ya shilingi bilioni 8.6.
Kupitia kipindi cha SupaMix cha EA Radio, Diamond alisema, “Ukiachilia mbali kazi ya muziki mimi pia nina vikorokoro kibao ambavyo vinaniwezesha kuweza kupata kipato cha kila siku.”
“Siyo kwamba muziki ni kila kitu lazima kujishughulisha na Mungu anasaidia kuweza kusonga mbele,” ameongeza staa huyo
No comments