TID bado ni kaka yangu, nampenda, namheshimu – Billnass
Kuna vita vikali vya maneno kati ya TID na aliyekuwa kijana wake, Billnass.
Hata hivyo Bill ambaye jina lake halisi ni William, haoneshi kutaka kumjibu TID, hataki makuu na ‘anaplay smart.’
“Kuna vitu vingi sana ila mimi sitaki kuzungumza sana, ninachoweza kusema ni kuwa nampenda TID na namheshimu,” rapper huyo alikiambia kipindi cha Super Mega cha Kings FM kinachoendeshwa na Divine Kweka.
Bill bado anasisitiza kuwa mkataba wake, hata kama ulikuwa wa maneno ulimalizika baada ya mwaka mmoja na alikuwa huru kwenda popote. Anasema hawezi kuongea na TID moja kwa moja lakini ameshaongeza na watu anaowaheshimu ili waongee na bosi wake huyo wa zamani ili wayaache yaliyopita yapite na wasichafuliane kwenye vyombo vya habari.
No comments