Header Ads

Header ADS

Roma-Nilitaka kumkumbusha Babutale asisahau alikotoka


Bosi kagamnda Dangote kaisahau Tip Top,” ni mstari wa Roma kwenye wimbo wake mpya ‘Kaa Tayari’ uliogeuka kuwa maarufu zaidi                                                                                                                                                .Ni mstari uliomlenga meneja wa Tip Top, Babutale ambaye miaka ya hivi karibuni amekuwa karibu zaidi na Diamond ambaye pia ni meneja wake.
“Nilichojaribu kumaanisha ni kwamba tusisahau tulikotoka ni kwasababu kuna watu walikuwa wanatutazama, kuna watu walikuwa wanafaidika na kule ambako tumetoka kwahiyo hata baadaye tunakuja kupata mafanikio na kuwekeza nguvu sehemu nyingine, asili kule nyumbani kulikotulea kukatufanya tuwe watu fulani hatupaswi kupasau,” Roma ameiambia Bongo5.
Roma amesema watu wanaweza wasimwelewe sasa hivi lakini anachoamini ni kuwa inaweza ikasaidia Tip Top ikaamka tena na kuwa kama zamani.
“Credit zitarudi tu kwamba Roma alisaidia, alimkumbusha bosi,” ameongeza.

No comments

Powered by Blogger.