Header Ads

Header ADS

Mourinho kuamua nafasi ya Rooney Uingereza

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho ataamua ni safu gani ambayo Wayne Rooney atalichezea taifa lake ,kulingana na mkufunzi mpya wa Uingereza sam alladyce


                    Rooney mwenye umri wa miaka 30 alicheza safu ya mashambulizi chini ya mkufunzi Roy Hodgson katika michuano ya Euro 2016
           Lakini Allardyce amesema kuwa ni mapema mno kuthibitisha iwapo Rooney,ambaye analiongoza taifa lake katika ufungaji wa mabao atasalia kuwa nahoda wa timu hiyo.


''Nadhani Wayne Rooney bado ana fursa kubwa kuchezea Uingereza'', alisema mkufunzi yo mwenye umri wa miaka 61
                                                                                                                                                                       ''Iwapo Jose atasema kwamba hatamchezesha katika safu ya kati na anamchezesha katika eneo la mashambulizi katika klabu ya Manchester United,itakuwa haina maana yoyote mimi kumchezsha katika safu ya kati''

No comments

Powered by Blogger.