Header Ads

Header ADS

Mourinho amtoa hofu Rashford baada ya ujio wa Ibrahimovic Old Traford

Kocha mpya wa timu ya Manchester United, Jose Mourinho amevunja uvumi ulioenea juu ya nafasi ya Marcus Rashford baada ya kusajiliwa Zlatan Ibrahimovic.                      CityMourinho amesema kuwa Rashford na Ibrahimovic watacheza kwa pamoja kwenye safu ya ushambuliaji ya Manchester United kwa msimu ujao utakaoanza Agosti 13 mwaka huu.
Rashford (18) ameonekana kufanya vizuri akiwa na United kuanzia mwishoni mwa msimu alipoanza kuchezeshwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Louis Van Gaal na kufanikiwa kufunga jumla ya magoli matano katika mechi 11 alizocheza akiwa na timu hiyo hali iliyomvutia mpaka aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza kumuita kwenye kikosi cha timu hiyo ya taifa kilichoshiriki michuano ya Uero.
“Ngoja nianze na jambo moja. Miaka 34 ndio umri wa Zlatan, na Marcus 18 – 34 jumlisha 18 gawanya kwa mbili ni umri safi kabisa wa mcheza soka,” Mourinho aliiambia MUTV. “Hawa ndio washambulizi wetu, wapo katika umri sahihi kwa sababu 18 si umri sahihi na 34 siyo. Naamini watashabihiana vema kulingana na ubora wao.”
Ibrahimovic amemzidi Rashford miaka 16 na amesajiliwa na United kwenye majira haya ya kiangazi akitokea kwenye timu ya PSG kwa uhamisho huru.

No comments

Powered by Blogger.