Model wa Tanzania Herieth Paul akava jarida la Flare la Canada
Supermodel wa Tanzania, Herieth Paul amekava jarida la Flare la Canada.
Herieth aliyezaliwa Dar es Salaam, alihamia nchini Canada miaka kadhaa iliyopita baada ya mama yake anayefanya kazi za kidiplomasia kuhamishiwa nchini humo. Kwa sasa anafanyia kazi zake jijini New York, Marekani.
Mwaka huu alichaguliwa kuwa kisura wa brand maarufu sana ya urembo duniani, Maybelline na kuungana na masupermodel wengine wakiwemo Gigi Hadid na Jourdan Dunn na wengine.
No comments