Header Ads

Header ADS

Man Utd nambari tano kwa utajiri duniani

Klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza imeorodheshwa ya tano kwa utajiri duniani na jarida la Forbes, thamani yao ikiwa imepanda kwa asilimia saba                   SPT_GCK_170516_Barclays Premier league. Manchester United v AFC Bournemoth. Picture Graham Chadwick. Rooney is congratulated after making it 1-0Klabu ya NFL, Dallas Cowboys, ndiyo inayoongoza thamani yake ikiwa $4bn (£3.03bn), na ni mara ya kwanza kwa klabu ambayo haichezi kandanda kuongoza katika orodha hiyo tangu kuanzishwa kwake 2011.
United, walioongoza orodha hiyo 2011 na 2012, wana thamani ya $3.32bn (£2.52bn).
Real Madrid ni wa pili kwa $3.65bn (£2.77bn) na Barcelona wa tatu $3.55bn (£2.69bn).
United, klabu pekee ya Uingereza katika orodha hiyo, walisaidiwa sana na mkataba wao wa £750m na Adidas, jambo lililoongeza thamani yao licha ya kushindwa kufuzu kwa michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Hata hivyo, Manchester United, ndio wenye deni kubwa zaidi miongoni mwa klabu zilizo katika 25 bora.
Arsenal (23), Manchester City (28), Chelsea (36) na Liverpool (41) ndizo klabu hizo nyingine za Uingereza zilizofanikiwa kuwa kwenye orodha hiyo.

No comments

Powered by Blogger.