Familia ya dereva wa mbio za magari wa SA aliyefariki akikwea Mlima Kimanjaro yazungumza
Lakini amesema wakati mwanae amemkumbatia kumuaga kuja Tanzania kupanda mlima huo, Peter Zulu hakuwaza kuwa ndio alikuwa akimuaga mara ya mwisho na kwamba sio magari yatakayochukua uhai wake, bali kupanda mlima.
Gugu aliyekuwa na miaka 38 alifariki Jumatatu iliyopita wakati akijaribu kupanda Mlima Kilimanjaro kama sehemu ya mradi wa Trek4Mandela wenye lengo la kukusanya fedha kusaidia wasichana zaidi ya 350,000 wasiojiweza.
Mwili wake uliwasili Alhamis iliyopita nchini humo.
Mjomba wake na Gugu na msemaji wa familia hiyo, Tseliso Motloheloa, alisema kuwa mazishi ya Gugu yatafanyika Alhamis hii kwenye kanisa la Rhema.
Motloheloa alisema post-mortem ilifanyika Tanzania na kwamba familia haijaamua kama wanataka ifanyike nyingine Afrika Kusini.
Wazazi wake wamedai kuwa hakuna wanayemlaumu kwa kifo cha mtoto wao.
No comments